KITUO cha Afya Makole kinakabiliwa na changamoto ya uzio wa kudumu kuzunguka kituo hicho kilichopo mjini Dodoma licha ya mafanikio katika kuboresha miundombinu na utoaji huduma kwa wananchi.
Kauli hiyo iliyolewa na Mganga Mfawidhi wa kituo cha Afya Makole, Dkt. George Matiko alipokuwa akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya mradi wa ujenzi wa majengo matano katika kituo hicho mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC).
Dkt. Matiko alisema “changamoto zinazokabili kituo cha Afya Makole ni pamoja na ukosefu wa uzio wa kudumu kuzunguka kituo. Ukosefu wa jengo maalum kwa ajili ya kufulia na kunyooshea nguo”. Changamoto nyingine aliongeza kuwa ni ukosefu wa jenereta lenye uwezo wa 25 KV ili kutumika kwa majengo yote kama dharura endapo umeme wa TANESCO utakatika, aliongeza. Nyingine ni kuchakaa kwa gari la kubebea wagonjwa kutokana na kutumika kuhudumia vituo viwili vya Afya na Zahanati 11.
Kituo cha Afya Makole kilianzishwa mwaka 1978 hivi sasa kina watumishi 135, kikihudumia zaidi ya wananchi 21,400 kikiwa na vitanda 45.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.