MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Stanslaus Mabula amelipongeza jiji la Dodoma kwa kutengeneza vitega uchumi mbalimbali vya kudumu vyenye lengo la kuimarisha mapato ya Jiji hilo.
Mabula ametoa pongezi hizo wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa kupitia fedha za Boost, mapato ya ndani na fedha kutoka serikali kuu ambapo katika ziara hiyo aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma pamoja na Sekretarieti yake na wataalamu kutoka Halmashauri ya Kongwa na Jiji la Dodoma.
"Majiji mengi hayana miradi kama hii Dodoma ni jiji changa lakini mnakua kwa kasi na kazi yenu inaonekana machoni hongereni kwa kazi nzuri. Miradi kama hii inahitaji wawekezaji wazuri ili iendelee kuwanufaisha kwahiyo inatakiwa mfanye jitihada ili ifanye kazi vizuri hongereni na msichoke kuendelea kuwekeza na kuwaza miradi mikubwa zaidi," alisema Mabula
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule alisema uwepo wa miundombinu hiyo (Ukumbi wa mikutano na Hoteli ya Jiji) unawarahisishia ufanisi wa kazi wageni wanaofika Mkoani hapo kwa lengo la kuwekeza na kupata huduma za Kiserikali na kuwataka uongozi wa Jiji kuendelea kuweka vivutio vya kisasa vinavyoendana na miundombinu hiyo.
"miundombinu bora inahitaji vivutio vya kisasa ili kuendana na makao makuu ya nchi, uwepo wa ukumbi huu wenye uwezo wa kubeba watu 1000 utarahisisha kufanyika kwa vikao vya kitaifa na kimataifa pia uwepo wa Hoteli ya Jiji umerahisisha angalau mabalozi na watu wengine wanaohitaji kupumzika kwenye hoteli yenye hadhi ya nyota tano kwasababu hoteli hii angalau inakaribia kufikia hadhi hiyo", alisema Senyamule.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.