KAMATI ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imepongeza ujenzi wa majengo matano katika kituo cha Afya Makole jijini Dodoma ikiwa ni mkakati wa serikali wa kuboresha huduma za Afya nchini.
Pongezi hizo zilitolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Vedasto Ngombale alipoongoza wajumbe wa kamati hiyo kutembelea kituo hicho cha Afya kilichopo katikati ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma jana.
Ngombale alisema kuwa kazi iliyofanyika ni nzuri iliyolenga kuboresha huduma za Afya katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Mjumbe wa Kamati hiyo, Selemani Zeddy aliwapongeza wabunge kwa kupitisha shilingi 500,000,000 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa kituo hicho. “Mheshimiwa Mwenyekiti napenda kuwapongeza waheshimiwa wabunge kwa kupitisha fedha hizo kuja hapa” alipongeza Zeddy. Aidha, alitaka ufafanuzi wa hali ya utoaji huduma baada ya fedha hizo kufika katika kituo cha Afya Makole.
Akijibu hoja hiyo, Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Dkt. George Matiko alisema kuwa wigo wa utoaji huduma umeongezeka na kuwa bora zaidi kwa ongezeko la majengo kutoka matano hadi kufikia 10. “Jengo la wodi ya kina mama wajawazito limehudumia wateja waliojifungua kawaida 8,211 toka mradi ulipokamilika mwezi Julai, 2018. Jengo la upasuaji zimefanyika huduma za upasuaji wa dharura kwa wateja 1,054” alisema Dkt. Matiko.
Mafanikio mengine aliyataja kuwa ni ongezeko la baadhi ya huduma kama maabara na kupunguza mlundikano wa wateja kusubiri huduma hiyo. “Tumeweza kupata mashine za kupima 'full blood picture' na mashine ya 'ultrasound'. Mpaka sasa kitengo hicho kimehudumia wateja 4,174’’ aliongeza Dkt. Matiko.
Ikumbukwe kuwa kituo cha Afya Makole kilianzishwa mwaka 1978 na kusajiliwa kwa namba 028.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.