JUMLA ya kompyuta mpakato (Laptop) 287 zimetolewa na shirika la CAMFED (Campaign for women Education) kwa ajili ya wanafunzi wa kike 287 wa kozi ya Stashahada ya Uuguzi na Ukunga.
Akipokea kompyuta hizo katika hafla fupi iliyofanyika leo jijini Dar Es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi amelipongeza shirika hilo kwa kuendelea kusaidia wanafunzi wanaotoka katika familia duni hususani watoto wa kike.
Prof. Makubi amesema shirika hilo linalipia wanafunzi hao ada ya miaka mitatu ya masomo pamoja na kuwapatia fedha za kujikimu na malazi lengo likiwa ni kuwainua watoto wa kike kielimu wanaotoka kwenye familia zisizojiweza katika kada mbalimbali ili waweze kujikimu kimaisha.
Aidha, Prof. Makubi amewataka wanafunzi hao kutumia nafasi hiyo kikamilifu kwa kusoma kwa bidii na kuzingatia maadili ya kitaaluma.
Prof. Makubi amelitaka shirika la CAMFED kuendeleza mradi huo ili wanafunzi wengi waweze kunufaika huku akisema kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki na kutoa ushirikiano ili kutimiza lengo la kuwasaidia wanafunzi wengi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.