SHIRIKA lisilo la kiserikali la 'LEAD Foundation' limesema limejidhatiti kurudisha uoto wa asili jijini Dodoma ili kuendeleza juhudi za kuhifadhi mazingira kutokana na mabadiliko ya tabia nchi duniani.
Hayo yalisemwa na Samwel Msanjila ambaye ni Mratibu wa Mradi wa Kinga Maji alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la shirika hilo katika Maonesho ya Nanenane Jijini hapa.
Alisema kuwa, mikoa yenye hali ya ukame kama Dodoma mradi wa kingamaji ni muhimu kwa ajili ya kuvuna maji mengi kwa matumizi ya kilimo.
"Na haya makinga maji unayoyaona tunayafanya katika shambani na si kama yale yanayowekwa majumbani" alisema.
"Licha ya kutumika katika mashamba tunarudisha rutuba katika mashamba tunazuia mmomonyoko wa ardhi na kurudisha uoto wa asili" aliongeza.
Amesema makinga maji hayo yanategeshwa mashambani katika msimu wa mvua ili kuweza kuvuna maji na moja kati ya mfano walioufanya wa makinga maji hayo ni katika kijiji cha Pemba Moto kilichopo wilayani Kongwa.
Shirika hilo lilianzishwa miaka kumi iliyopita na askofu mstaafu kanisa la Anglican Mpwapwa Simoni Chiwanga likiwa na lengo la kusimamia mafunzo ya usimamizi wa mazingira, mafunzo ya uongozi bora na miradi midogo ya maendeleo ya jamii.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.