MWENGE wa Uhuru unalenga kuchochea maendeleo na kukumbusha amani, upendo, mshikamano na kudumisha Muungano wilayani Dodoma.
Kauli hiyo ilitolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge maalum wa Uhuru mwaka 2021, Lt. Josephine Mwambashi katika mapokezi ya Mwenge huo eneo la Makutopora wilayani Dodoma.
Lt. Mwambashi alisema “ndugu zangu wa Wilaya ya Dodoma, Mwenge maalum wa Uhuru unakuja wilayani Dodoma kuchochea maendeleo. Mwenge unatukumbusha kulinda amani, upendo, mshikamano, umoja wa kitaifa na kudumisha Muungano”.
Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge kitaifa alitoa angalizo kwa uongozi wa Wilaya ya Dodoma. Alisema kuwa Mwenge huo utakapokuwa unakimbizwa wilayani Dodoma, nyaraka zote za miradi zikutwe eneo la mradi pamoja na wahusika wote katika miradi hiyo. Angalizo lingine alilolitoa ni kupatiwa taarifa zote za miradi kabla ya kuanza mbio za Mwenge maalum wa Uhuru wilayani humo.
Kuhusu mbio za Mwenge maalum wa Uhuru wilayani Kondoa, Lt. Mwambashi alisema kuwa miradi yote iliyopitiwa na Mwenge maalum wa Uhuru iwe chachu ya utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo wilayani Kondoa.
Mwenge maalum wa Uhuru umepokelewa wilayani Dodoma leo ukitokea Wilaya ya Kondoa na utakimbizwa zaidi ya kilometa 100 na kupitia miradi mitano ya maendeleo. Mwenge maalum wa Uhuru unaongozwa na kaulimbiu isemayo “TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu; itumie kwa usahihi na uwajibikaji”.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.