• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Lukuvi ashusha gharama za urasimishaji, wanaoishi mijini sasa hati ni lazima

Imewekwa tarehe: August 17th, 2021

Na. Munir Shemweta, DODOMA

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ametangaza kupunguzwa gharama za urasimishaji makazi holela kutoka shilingi 150,000 hadi 130,000 na kusema kila mmiliki wa ardhi anayeishi mjini sasa lazima awe na hati.

Aidha, Waziri Lukuvi amesema wananchi wasio na uwezo wa fedha kwa ajili ya zoezi hilo sasa watakopeshwa na Benki ya NMB ambayo imeingia makubaliano na Wizara ya Ardhi kwa ajili ya zoezi hilo.

Amesema, si suala la hiyari mmiliki wa ardhi kuwa na hati bali ni lazima na kubainisha kuwa katika kipindi cha miezi mitatu taratibu za kutambua maeneo ya urasimishaji zifanyike ili kuanza zoezi.

Zoezi la urasimishaji makazi holela limenzishwa kwa ajili ya kutambua maeneo yaliyojengwa kiholela bila kufuata taratibu za mipango miji na zoezi hilo lilianza mwaka 2013 na kutarajiwa kukamilika 2023.

Awali katika katika zoezi hilo, wananchi walitakiwa kulipia kwa viwango tofauti kuanzia shilingi 250,000 hadi 350,000 na baadaye Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alipunguza hadi kufikia shilingi 150,000.

Akizungumza na makampuni ya upangaji, upimaji na watendaji wa sekta ya ardhi mkoani Dodoma leo tarehe 17 Agosti 2021, Waziri Lukuvi amesema, zoezi hilo ni la lazima na kila mwananchi mwenye nyumba au kiwanja anayeishi mjini lazima awe amemilikishwa na kupatiwa hati.

"Uhamasishaji lazima ufanyike ili wananchi wajue kama wanapaswa kuingia katika zoezi hilo na kuelewa umuhimu wa upatikanaji miundombinu. Mfumo wa ukusanyaji na utumiaji fedha za urasimishaji makazi holela katika maeneo mbalimbali haukuwa mzuri na kwa kiasi kikubwa umekwamisha zoezi kwenda kwa kasi. Tumekwama muda mrefu katika urasimishaji na sasa tumekubaliana na Benki ya NMB iwakopeshe na kulipa kwa riba ya asilimia 10" amesema Lukuvi.

Aidha, Waziri wa Ardhi aliwataka watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri za wilaya kuanza kutambua na kuainisha makampuni yatakayofanya kazi za urasimishaji kwa kuangalia uwezo wa kila kampuni na kuunda kamati ya urasimishaji ya mtaa na kuanza zoezi.

"Mtakaoenda kufanya kazi lazima mfanye tathmini ya kazi au miradi iliyofanyika kwenye maeneo yenu ili kuona kazi zilizofanyika na zile zilizoshindwa kufanyika" amesema Lukuvi.

Akifafanua zaidi, Lukuvi alisema baada ya kukamilika zoezi la utambuzi, Benki ya NMB itatoa mkopo wa shilingi 130,000 na katika fedha hizo kampuni itapewa 120,000 huku 6,000 ikienda halmashauri kwa ajili ya miundombinu ya barabara na nyingine ikibaki kwa halmashauri kwa ajili taratibu za hati.

Hata hivyo, Lukuvi alitoa angalizo kwa kusema kuwa, kuna baadhi ya mitaa wananchi wake tayari wameshatoa fedha kwa ajili ya zoezi la urasimishaji hivyo watendaji wa sekta ya ardhi wanatakiwa kufanya ukaguzi ili wananchi wasije kutoa fedha mara mbili.

"Nitoe angalizo kule katika mitaa kuna fedha zimetolewa na baadhi ya wananchi kwa ajili ya urasimishaji hivyo mkafanye ukaguzi ili wananchi wasije kuchangishwa mara mbili na hili, siyo zoezi jipya na kama mtu ametoa 70,000 basi iongezwe ili itimie 130,000 na fedha zote zipitie benki ya NMB na mkopo utarejeshwa katika kipindi kisichozidi miezi 24" amesisitiza Lukuvi.

Vile vile, Waziri Lukuvi amesema ni lazima wananchi wakopeshwe fedha ili wakalipie gharama zote za urasimishaji na kuwataka watendaji wa sekta ya ardhi kuwa mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wanapata na hati sambamba na kila mtaa kuwa na uhakika miundombinu ya barabara.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Makazi Wizara ya Ardhi, Deogratias Kalimenze amezitaja baadhi ya changamoto zilizochangia kuzorota kwa zoezi hilo kuwa ni uhaba wa fedha za utekelezaji miradi, kampuni kuwa na mitaa mingi kuliko uwezo, uchangiaji fedha usioridhisha pamoja na baadhi ya kampuni kutokuwa na mitaji.

Kwa Mujibu wa Kalimenze changamoto nyingine ni ufuatiliaji hafifu kwa baadhi ya watendaji wa sekta ya ardhi, baadhi wananchi kukataa kuachia maeneo kwa ajili ya huduma za jamii pamoja na baadhi ya ofisi kuchelewesha kazi za uidhinishaji michoro.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.