WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ameyataka Mashirika, Makampuni na Taasisi zinazodaiwa Kodi ya Ardhi kuhakikisha zinalipa kodi hiyo ifikapo Juni 20 , 2019 vinginevyo zitafikishwa katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba na huko hatua za kufuta umiliki pamoja na kutaifisha mali za kufidia madeni itafanyika.
Lukuvi alisema hayo tarehe 11 Juni 2019 alipokutana na wawakikishi waMashirika, Makampuni na Taasisi zinazodaiwa madeni makubwa ya kodi ya Ardhi katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
Alisema, ulipaji kodi ya pango la ardhi ni takwa la kisheria na kila mmiliki anawajibika kulipa kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha ili kuepuka riba na kusisitiza kuwa hatua kwa wasiolipa kodi na wadaiwa sugu ni kuwafikisha mahakamani na zoezi litaanza tarehe 21 Juni 2019.
“Mtambue ulipaji kodi ya ardhi si jambo la hiari unawezesha Serikali kutekeleza Bajeti ya nchi ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli pamoja na kutoa huduma mbalimbali za jamii “ alisema Lukuvi
Kwa mujibu wa Waziri Lukuvi, watakaoshindwa kulipa kodi ya pango la ardhi baada ya muda kuisha hatua za kufuta miliki zao, kunadi mali na kuuza viwanja husika itafuta.
Waziri Lukuvi alisema, Serikali inadai kiasi kisichopungua bilioni 200 kutoka kwa wadaiwa 207 ambao ni Mashirika, Taasisi na Makampuni na kuongeza kuwa orodha ya wadaiwa wengine itatolewa karibuni.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.