Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ametoa kibali cha kuajiri madaktari wapya 1,000 ili kutatua changamoto ya uhaba wa wataalam hao wa afya nchini.
Kiongozi mkuu huyo wa nchi ametoa kibali hicho jana Alhamisi Februari 20, 2020 katika mkutano wa madaktari pamoja na watumishi wa sekta ya afya uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
“Ninafahamu kuna madaktari karibia 2,700 hawajaajiriwa, nitalifanyia kazi. Nafikiri tunaweza tukaanza polepole hata tukachukua 1,000 eti Waziri wa Utumishi (George Mkuchika) hatuwezi kuajiri hata 1000,” alihoji Rais Magufuli.
“Hela si zipo kidogo? Basi tuajiri madaktari 1,000. Tuanze na 1,000 mambo yakiwa mazuri tena tunaajiri wengine kwa sababu tunahitaji madaktari mpaka vijijini.”
Amesema madaktari hao wanatakiwa kuajiriwa ili kupata uzoefu wa vifaa vipya vinavyoingia nchini, “hawa madaktari 1,000 waajiriwe wakapate experience (uzoefu) ya mavifaa haya yanayokuja na wagawanywe vizuri katika mikoa yote.”
Aidha, Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT) kwa kutambua mchango mkubwa wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika sekta ya afya nchini walimtunukia tuzo Maalumu aliyokabidhiwa na Rais wa Chama cha Madaktari Dkt. Elisha wakati wa Maadhimisho hayo ya Siku ya Madaktari Kitaifa mwaka 2020 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam Februari 20, 2020
Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokeTuzo Maalumu aliyokabidhiwa na Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT) kwa kutambua mchango wake Mkubwa katika sekta ya Afya nchini toka kwa Rais wa Chama hicho Dkt. Elisha wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Madaktari Kitaifa mwaka 2020 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam Februari 20, 2020
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.