• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Maadhimisho siku ya UKIMWI Duniani kufanyika Lindi

Imewekwa tarehe: November 15th, 2022

WAZIRI wa Nchi Ofisi Ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene amesema maadhimisho ya siku ya UKIMWI yanatarajiwa kufanyika Mkoani Lindi katika Uwanja wa Ilulu.  Simbachawene ametoa taarifa hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Ngome, Jijini  Dodoma.

Amesema kuwa maadhimisho hayo yataambatana na maonesho ya shughuli mbalimbali kutoka kwa wadau wa UKIMWI zikiwemo  huduma ya upimaji wa hiari wa virusi vya UKIMWI na magonjwa mengine  itakayotolewa kuanzia   Novemba  24 hadi Desemba  01, 2022.

“Kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Imarisha Usawa’ ambayo imetafsiriwa kutoka kauli mbiu ya kimataifa 'equalize', kaulimbiu hii inahimiza kutilia mkazo uimarishaji wa usawa kutoa huduma za UKIMWI kwa makundi yote ya wananchi na katika maeneo yote ya kijeografia kwa kuondoa vikwazo vinavyoondoa usawa katika kufikia dira ya kutokomeza UKIMWI ifikapo mwaka 2030.” Amesema Simbachawene.

Pia ameeleza kwamba maadhimisho hayo yatatumika  kutathimini hali halisi na muelekeo wa kudhibiti virusi vya UKIMWI, Kitaifa na Kimataifa pamoja na kuhamasisha viongozi na jamii kuendelea kwa mapambano  ya kudhibiti virusi vya UKIMWI ili  kujumuisha katika mipango yao ya maendeleo.

“Maadhimisho haya yatatumika kama sehemu ya kuwaenzi wahanga wanaoishi na virusi vya UKIMWI na kuwakumbuka wale waliopoteza maisha  kutokana na UKIMWI pamoja na kujali yatima  ambao wametokana  na vifo vilivyosababishwa na ugonjwa huo.

Vilevile Simbachawene ameiagiza  Mikoa yote nchini kuandaa na kuadhimisha siku hiyo kwa kushirikiana na wadau wengine katika  Mikoa na katika ngazi ya Wilaya.

“Maadhimisho haya yatatumika kuhamasisha masuala mabalimbali muhimu ikiwemo  utekelezaji wa azimio la umoja wa mataifa  la kutokomeza UKIMWI katika kuhakikisha  afua za kiafya  zinapewa rasilimali za kutosha na mifumo ya kiafya inaimarishwa”Amebainisha Simbachawene

Aidha amesema kuendelea kuwepo kwa siku hiyo muhimu kutasaidia  upatikanaji wa dawa za kufubaza VVU, kuendeleza utafiti wa kutafuta chanjo, kuimarisha afua za kinga dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI na kuendelea kutekeleza afua za UKIMWI kwa kuzingatia na kuheshimu haki za binadamu.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.