Na. Asteria Frank, DODOMA
Wizara ya mifugo kushirikiana Halmashauri ya jiji la Dodoma wameadhimisha siku ya kichaa cha mbwa duniani kwa lengo la kuelimisha juu ya udhibiti wa ugonjwa wa kichaa cha mbwa Pamoja na kutowa chanjo kwa paka na Mbwa
Maadhimisho hayo yamefanyika katika ofisi za kituo za huduma za mifugo kanda ya kati Dodoma mjini ambapo wamefahamisha kuhusu kichaa cha Mbwa Pamoja na kutoa chanjo, dawa ya kuzuia viroboto na dawa za Minyoo kwa Mbwa na Paka.
Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Hussein Nyenye alisema kuwa ni muhimu kwa wafugaji wa mw ana paka kushirikiana na wizara ya mifugo ili kuweza kuwapatia mbwa na paka chanjo kwa wakati sahihi kuzuiya magojwa ,mbalimbali kwa Wanyama hao na wao wenyewe.
Alisema kuwa shughuli ya kudhibiti kichaa cha mbwa haiwezakani kufanyika na watu wa mifugo peke yake bali kwa ushiriki wa Sekta zingine kama Sekta ya Maendeleo ya Jamii, Sekta ya Afya na Sekta ya Elimu na ndio maana maafisa wanatowa elimu hii hata mashuleni kwa Watoto wetu na jamii kiujumla ili waweze kujikinga na ugonjwa wa kichaa cha mbwa.
“lakini wakati huohuo tunatowa elimu kwa wafugaji juu ya ufugaji bora wa mbwa, mbwa kwa kawaida anatakiwa afugwe ndani na apewe tiba ikiwa ni Pamoja na chanjo ya kichaa cha mwa, dawa za minyoo na dawa za kuzuiya wadudu kama viroboto ,kupe na kadhalika ambao wanaleta usumbufu wa wanyama na sio mbwa kudhurura mitaani” alisema Nyenye.
Kaimu Afisa Mfawidhi kituo cha huduma za mifugo kanda ya kati Dkt Dioniz Ibrahim alisema kuwa maadhimisho ya kichaa cha mbwa yanafanyika tarehe 28 septemba duniani Pamoja na kuongeza uwelewa juu ya udhibiti wa ugojwa wa kichaa cha mbwa.
Dkt Dioniz Ibrahim ambae pia ni daktari wa Wanyama wa mifugo kanda ya kati ambacho maarufu kinaafaamika kama ZVC ‘Zonal Venterinary Center’ Dodoma alisema kuwa hiki ni kituo ambacho kipo chini ya wizara ya mifugo na uvuvi ambacho kinaudumia mikoa miwili ambayo ni mkoa wa Dodoma na mkoa wa Singida ambayo majukumu yake makuu ni udhibiti wa magonjwa ya wanayama ikiwemo kichaa cha mbwa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.