Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, yaagiza Mikoa yote Nchini Pamoja na Mamlaka ya upangaji wa Makazi, kusimamia kikamilifu zoezi la utambuzi, upangaji, upimaji na umilikishaji wa makazi kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyotolewa ili kila mwananchi mwenye kiwanja na nyumba sehemu zinazokubalika kisheria aweze kukamilishiwa umiliki wake.
Maagizo hayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge aliyemuwakilisha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi katika Maadhimisho ya siku ya Makazi Duniani yaliyofanyika Kitaifa Mkoani hapa.
Dkt. Mahenge alisema, ili kuweka mazingira ya nyumba kuwa bora na ya kuvutia ni wajibu wa kila mwananchi kuzingatia kanuni ya kuchangia sehemu ya ardhi yake kwa ajili ya huduma za kijamii katika maeneo yao.
Aidha alizitaka Halmashauri zote nchini kuwapatia waendelezaji milki huduma watakazohitaji kama vile kuainisha maeneo yaliyoiva kimipangomiji, kupima viwanja na kuweka miundombinu ya barabara, maji na umeme ili kurahisisha shughuli mbalimbali za kimaendeleo katika maeneo hayo.
“Halmashauri zinapaswa kutoa hati milki za ardhi na vibali vya ujenzi kwa wakati bila kusahau jukumu lao la msingi la kusimamaia na kukagua utekelezaji wa miradi ya mbali mbali ya ujenzi” Alisema Dkt. Mahenge.
Siku ya Makazi Duniani huazimishwa kila Jumatatu ya kwanza ya mwezi wa kumi, ambapo kitaifa maadhimisho hayo yamefanyika Mkoani Dodoma yakiwa na kauli mbiu inayosema “Nyumba kwa wote: kwa Miji bora ya baadae”
Washiriki wa Maadhimisho ya Siku ya Makazi Duniani yaliyofanyika kitaifa hapa Jijini Dodoma wakimsikiliza mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge (hayupo pichani) aliyemwakilisha Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.