Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika kwa Mkoa wa Dodoma yamefanyika leo Juni 16, 2018, katika viwanja vya Shule ya Msingi Kikuyu Kusini iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Mgeni rasmi katika Sherehe hizo alikuwa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Deo Ndejembi ambaye aliwakilishwa na Diwani wa Kata ya Kikuyu Kusini Anselem Kutika ambaye alitoa wito kwa wadau na mamlaka mbalimbali kuzidisha juhudi katika kulinda haki za mtoto.
Katika sherehe za maadhimisho hayo iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali, watoto ambao ndio walengwa wakuu walipata nafasi ya kuonyesha vipaji mbalimbali kama vile kucheza Sarakasi na uimbaji.
Baadhi ya wadau ikiwemo Taasisi inayojishughulisha na masuala ya Vijana ya DOYODO wameshiriki na kutoa elimu ya Uzazi na Mimba za utotoni kwa watoto wa kike kwa lengo la kumkomboa mtoto wa kike kuepukana na janga la mimba za utotoni ili atimize ndoto zake katika maisha ikiwemo kupata Elimu.
Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Mufungo Manyama aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi alisema, kwa mwaka huu maadhimisho hayo yameambatana na kauli mbiu isemayo "Kuelekea uchumi wa viwanda, tusimwache mtoto nyuma".
(Picha kwa hisani ya DOYODO)
Mkurugenzi wa taasisi ya DOYODO Rajabu Juma Nh'unga akitoa mada wakati wa maadhimisho.
Baadhi ya watoto wakifuatilia Elimu iliyokuwa ikitolewa ili kuwajenga watoto juu ya haki zao na wajibu wao kwa Jamii na Taifa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.