Maafisa elimu kata na walimu wa TEHAMA wapatiwa mafunzo
Imewekwa tarehe: January 1st, 2025
OR-TAMISEMI
MAAFISA Elimu Kata 128 pamoja na waalimu wa TEHAMA 128 wamepatiwa mafunzo ya uelewa na ufahamu wa matumizi ya TEHAMA shuleni.
Mafunzo hayo ya siku nane yanafanyika katika shule ya Sekondari ya Wavulana Kibaha Mkoani Pwani kupitia programu ya Uboreshaji wa Elimu ya Awali na Msingi (BOOST).
Akielezea malengo ya mafunzo hayo Mwezeshaji kutoka Chuo cha Ualimu Tabora, Patrick Sitta alisema lengo kuwajengea ufahamu na uelewa waalimu na maafisa elimu kata kuhusu matumizi ya TEHAMA katika kufundisha na kujifunza.
Alisema mafunzo hayo yatajikita katika matumizi ya TEHAMA shuleni, utunzaji wa vifaa hivyo na namna ya kuongoza shule yenye vifaa vya TEHAMA pamoja na matumizi ya ubao janja.
Sitta anafafanua kuwa mafunzo hayo yanajumuisha utunzaji wa vifaa na pia yamezingatia mahitaji na mazingira ya shule.
Mikoa inayoshiriki kwenye mafunzo hayo ni Pwani, Lindi, Mtwara, Morogoro na Dar es Salaam