SERIKALI imewataka Maafisa Maendeleo nchini kuacha kutumia vyeo vyao kwa kuweka taarifa hewa za vikundi vya mikopo ya asilimia 10 kwa lengo la kujinufaisha.
Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Angellah Kairuki wakati akifunga kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka Sekretarieti za Mikoa na Wakuu wa Idara wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini, uliofanyika Jijini Dodoma, kuanzia tarehe 8 hadi 10 Novemba, 2022, katika Ukumbi wa hoteli ya Morena.
Kairuki amewaonya vikali Maafisa hao wanaotumia vibaya vyeo vyao wajilekebishe mara moja vinginevyo watakutana na mkono wa Dola kwa mujibu wa Sheria zilizowekwa.
"Naomba kama wapo ambao huko nyuma kabla ya leo tarehe 10, walikuwa na makandokando hayo tubadilike, ni tamaa ambazo hazina baraka na ni wizi wa kuwaibia walipa kodi na wanasononeka, machozi yao hata siku moja hayatakufikisha sehemu salama" amesema Kairuki.
Kairuki amesema hatarajii kuona kesi baada ya tarehe ya leo, wala kusikia kesi za Manispaa mbalimbali kama vile Manispaa ya Ilala, Kinondoni na Kalambo kuanza kupokea kesi wakati maelekezo yalikwishatolewa na Katibu Mkuu wakati wa kikao kazi.
Aidha, amezitaka Halmashauri nchini kuendelea kutumia Mfumo wa kieletroniki wa mapato ya Asilimia 10 ili kuhakikisha kuwa Mikopo yote iliyotolewa na inayoendelea kutolewa inaratibiwa, kukusanywa kama madeni na kurejeshwa kwa wakati ili wengine wanufaike na mikopo hiyo.
"Naomba nisisitize fedha hizi ni mikopo inayotakiwa kurejeshwa na kuweza kuwakopesha wahitaji wengine, Halmashauri zote zihakikishe zinaweka Mikakati ya kukusanya madeni hayo na ifikapo mwezi Februari, 2023 nusu ya madeni hayo ambayo
yamepitwa na muda yawe yamerejeshwa na hatua sitahiki ziwe zimechukuliwa kulingana na Kanuni zilizopo” amesema Kairuki.
Akimkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula amewaasa Maafisa hao kufanya kazi kwa moyo, juhudi ni
maarifa lakini pia kutimiza wajibu wao kwenye maeneo yao ya kazi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.