WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema maagizo ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya nchi kujitosheleza kwa uzalishaji wa sukari yameanza kunukia baada ya uongozi wa kiwanda cha sukari cha Kagera Sugar kuongeza uzalishaji na kufikia tani 110,000 kutoka tani 60,000.
Ametoa pongezi hizo Oktoba 15, 2022 alipofanya ziara ya kukagua upanuzi wa mashamba ya miwa na mitambo na iliyoongezwa kwa ajili ya uzalishaji wa sukari katika kiwanda cha Kagera Sugar, Misenyi Mkoani Kagera.
Amesema kitendo cha kampuni hiyo kuendelea kuweka mikakati ya kuboresha na kukuza uwekezaji ni kizuri kwani kwa kiasi kikubwa kitawezesha kuongeza kiwango cha uzalishaji wa sukari nchini na kuipungua Serikali gharama ya kuagiza kutoka nje.
Kadhalika, Majaliwa amewahakikishia viongozi wa Chama cha Mapinduzi kuwa Serikali itaendelea kusimamia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwa lengo la kuhakikisha yale yote yaliyoahidiwa yanatekelezwa. "Viongozi wangu wa CCMsisi tutaendelea kumsaidia Rais Samia kuhakikisha yote yaliyoahidiwa yanatekelezwa."
Pia, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwahakikishia wawekezaji hao kwamba Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano ili malengo waliyoyaweka katika uwekezaji huo yaweze kufikiwa na kuongeza tija kwao na Taifa kwa ujumla.
Wakati huo huo, Majaliwa ametumia fursa hiyo kuiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuendelea kusimamia kikamilifu sharia za ukusanyaji wa mapato nchini.
"...Yeyote aliyeamua kufanya biashara nchini ahakikishe suala la kulipa kodi analipa kipaumbele. TRA chukueni hatua kwa mfanyabiashara atakayebainika kukwepa kodi."
Pia, Majaliwa ametumia fursa hiyo kuiagiza TRA
kuwafuatilia wafanyabiashara wanaotumia vibaya majina ya viongozi wakiwemo wa kitaifa kukwepa kodi wanazotakiwa kuzitoa kwa Serikali kwa kuwa kila anayefanya biashara nchini hata kama ni kiongozi anapaswa kulipa kodi.
"TRA endeleeni kuchukua hatua hata kwa kumfuata kiongozi aliyetajwa ili mjiridhishe kama kinachosemwa na mfanyabiashara ni sahihi, kwasababu matumizi mabaya ya
majina ya viongozi yanawasumbua sana watumishi wa TRA."
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.