KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na bunge) Bi. Dorothy Mwaluko (pichani juu) amesema kuwa kati ya vijana themanini (80) wenye maambukizi mapya, vijana sitini na nne (64) ni wasichana/wanawake.
Bi Dorothy Mwaluko ameyasema hayo wakati wa kilele cha maadhimisho ya kijiji cha vijana kuelekea siku ya UKIMWI Duniani itayofanyika tarehe 1 Disemba katika viwanja vya shule ya msingi Mandela kata ya Pasua Mkoani Kilimanjaro.
"Kati ya vijana themanini wenye maambukizi mapya, vijana sitini na nne ni wanawake au wasichana au katika watu 100, watu 80 ni wanawake au wasichana" ameyasema Bi. Dorothy Mwaluko.
Bi Dorothy Mwaluko amesema kuwa, kati ya Watanzania Milioni 60, vijana ni asilimia 68% huku zaidi ya asilimia 50% wakiwa ni wanawake/wasichana, huku akisisitiza kwa mazingira hayo yanaonesha kuangamia kwa walezi wa taifa letu.
"Kundi la vijana ni asilimia 68% ya watu takribani Milioni 60 ya Watanzania na kati ya hao, zaidi ya asilimia 50 ni wanawake, kwa muktadha huo, kundi la wanawake na wasichana ambao ndio walezi wa taifa hili wanaangamia, na kuangamia kwao ndio kuangamia kwa taifa letu" amesema.
Aidha, Bi Dorothy Mwaluko ametoa wito kwa vijana kupima na kujua hali zao, na kuanza kunywa dawa mapema pindi wagundulikapo kuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi, huku akitoa msisitizo kwa vijana kutokata tamaa pindi wakigundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Picha na matukio:
Chanzo: wizara_afya (instagram)
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.