WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mohamed Mchengerwa amesema mabaraza ya wafanyakazi ni chombo cha kisheria kinacholenga kuongeza tija na uwajibikaji mahali pa kazi.
Maelekezo hayo yametolewa jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Deogratius Ndejembi kwa niaba ya Waziri Mohamed Mchengerwa kwenye ufunguzi wa baraza la wafanyakazi wa ofisi ya Rais - TAMISEMI leo tarehe 13.03.2024.
“Mabaraza ya wafanyakazi yatumike kujadili malengo na mipango ya taasisi ikiwamo maslahi ya watumishi, mnatakiwa kujadili utendaji kazi wenu wa kila siku,”alisema.
Hata hivyo, alihimiza usimamizi wa mipango ya bajeti ili kufikisha huduma bora kwa wananchi.
Kadhalika, alisema serikali itaendelea kutatua kero zilizopo ikiwamo uhaba wa wafanyakazi.
Naye, Kaimu Katibu Mkuu, Dk.Charles Msonde alisema kikao hicho cha baraza pamoja na mambo mengine kitajadili na kupitisha bajeti ya ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa mwaka 2024/25.
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Dk.Wilson Mahera aliahidi watumishi wa TAMISEMI watatekeleza ipasavyo maelekezo yaliyotolewa na serikali.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.