Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi Halmashauri ya Jiji la Dodoma yafafanua mafanikio ya maboresho ya elimu katika shule za msingi ambayo inafanya ufaulu wa wanafunzi kuongezeka.
Ufafanuzi huo ulitolewa katika Mkutano wa Wadau wa Elimu na Utambulisho wa Mfuko wa Chakula na Lishe Shuleni ikiwa ni sehemu ya kujadili suala la lishe bora kuboreshwa kwa asilimia zote ili taaluma ya wanafunzi ifikie lengo tarajiwa.
Akizungumza katika mkutano huo, Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi, Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mwl. Prisca Myalla alisema “tunaishukuru serikali yetu kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kuboresha elimu na kujenga miundombinu mizuri ambayo kwasasa inasaidia utoaji wa elimu kuwa mzuri. Katika suala la lishe, tunashukuru mfuko wa chakula na lishe shuleni kwasababu unasaidia wanafunzi kuhudhuria shuleni hali inayopelekea mahudhurio kuwa juu ukilinganisha na kipindi cha nyuma”.
Akizungumza kuhusu hali ya ufaulu na jumla ya shule zilizopo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, alisema kuwa kuna jumla ya shule 194 ikiwa serikali inamiliki shule 107 shule mbili zikiwa za mchepuo wa kiingereza na shule za binafsi zikiwa 87. Idadi ya wanafunzi ni 112,699, mahitaji ya walimu ni 2,504 waliopo ni 1,993. Hivyo, Halmashauri ya Jiji la Dodoma ina upungufu wa walimu 511.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.