• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Mabwawa 16 kuondosha majitaka Jijini Dodoma

Imewekwa tarehe: January 22nd, 2021

SERIKALI ipo kwenye hatua za mwisho za kuhakikisha kunakuwepo na uondoshaji mkubwa wa maji taka katika Jiji la Dodoma unaojumuisha ujenzi wa kilomita 250 za mabomba pamoja na mabwawa 16 yatakayojengwa katika eneo la Nzuguni.

Hayo yamesemwa jana Januari 21, 2021 jijini hapa na Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Maryprisca Mahundi alipokuwa akifungua Baraza la Sita la wafanyakazi wa DUWASA ambapo amesema lengo ni kuifanya Dodoma kuwa na sura ya Makao Makuu ya nchi.

Amesema ili mradi huo ufanikiwe kwa malengo yaliyokusudiwa lazima wananchi wapatiwe elimu ya kutosha kwani ni wachache wanaofahamu kuwa wanaweza kuunganishiwa mfumo huo kutoka kwenye makazi yao hadi kupeleka maji taka kwenye mabwawa. 

"Duwasa inatakiwa kutatua kero kwani kero nyingine zimekuwa zikisababishwa na baadhi ya watu ambao wanashindwa kufanya kazi kwa ufanisi, baadhi ya wananchi wamekuwa wakilalamika kutokana na huduma wanazozipata hivyo kupitia baraza hili hakikisheni mnafanya kazi ya kuzitatua kero hizo ili wananchi wafurahie uwepo wa mtandao wa maji," amesema Waziri Maryprisca.

Amesema kuna kila sababu ya DUWASA kuendelea kuujenga mtandao wa maji kwa kuwafikishia wananchi huduma za maji kwani wanauhitaji huo. "Wizara itaendelea kuiwezesha ili iweze kutoa huduma bora kwa Wananchi," Amesema Waziri huyo.

Kwa upande wake Mhandisi Aron Joseph, Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya maji safi na Usafi wa Mazingira DUWASA amesema wao kama Mamlaka wataendelea kutoa huduma bora ya maji safi na Usafi wa Mazingira kwa wananchi wote wa Dodoma.

"Licha ya Dodoma kuongezeka watu kutokana na kutambulishwa rasmi kuwa ni jiji ili kukabili tatizo la ukosefu wa maji kwa wananchi, miradi ya muda mfupi na ya muda mrefu inahitajika ambapo katika mradi wa muda mfupi jumla ya visima 20 vimeanza kuchimbwa,

Mradi mkubwa katika Ziwa Victoria utakaopitia Mkoa wa Singida mpaka Mkoa wa Dodoma unatarajiwa kuwanufaisha wakazi wa Mikoa hiyo," amesema Muhandisi Aron.

Naye Mwenyekiti wa Bodi Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira DUWASA Faustine Bee amesema wamejipanga kupunguza malalamiko kwa wakazi wa Dodoma juu ya upatikanaji wa maji na Usafi wa Mazingira katika makazi yao.

Pia amesema wamejipanga kuhakikisha wanadhibiti upotevu wa maji kutoka asilimia 26 mpaka kufikia 10 au kumaliza kabisa tatizo hilo.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.