MADAKTARI bingwa kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa (Benjamin Mkapa Hospital) ya Jijini Dodoma wanaendelea kutoa huduma kwa wananchi wa Mkoa wa Singida kupitia Huduma ya Kliniki Tembezi wakishirikiana na Madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida.
Daktari bingwa wa Upasuaji wa Mifupa na ajali kutokea Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Charles Lema amesema wakishirikiana na madaktari wa idara zingine wanaendelea na Kliniki Tembezi mkoani Singida na kwa ujumla zoezi hilo linaenda vizuri.
Wakitoa ushuhuda wa jinsi walivyopata matibabu, baadhi ya wananchi wa Singida wameshukuru mno madaktari hao kutoka BMH kwa huduma zao na jinsi ambavyo wameweza kuwasaidia. Salum Athuman amesema alipata ajali ya pikipiki (bodaboda) tangu mwezi wa April. "Nilivyopata ajali ya pikipiki nikaletwa hospitali nikasafishwa kidonda na kushonwa, baada ya hapo nikaruhusiwa kwenda nyumbani, nikaambiwa nikae kama siku mbili nirudi tena. Nikakaa siku mbili hizo mguu ukawa unavimba nikarudi tena hospitalini, kuja kurudi hospitali mguu ukawa unatoa maji, na ile nyama iliyokuwa imeshashonwa ikawa imeoza. Nashukuru kwa Madaktari bingwa kutoka kwenye Hospitali ya Benjamin Mkapa wamekuja kutupatia tiba na mpaka sasa tunanafuu" alifafanua Athumani.
Salum Athumani akielezea shukurani zake kwa jinsi Madaktari bingwa wa Hospitali ya Benjamin Mkapa wakishirikiana na Madaktari bingwa wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida walivyosadia yeye na wananchi wengine wa Singida walivyosaidiwa kupata tiba.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.