WAZIRI wa MadiniDoto Biteko, amewataka wachimbaji wadogo wa madini nchini kuitumia Taasisi yaJiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kwa kutumia wataalam, vifaana taarifa za jiolojia zinazoandaliwa na GST katika kufanya shughuliza utafutaji, uchimbaji na uchenjuaji madini ili kufanya uchimbaji wenye tijakiuchumi na wenye kulinda mazingira.
Waziri Biteko amesemahayo leo Machi 11,2021 wakati akifanya uzinduzi wa kitabu cha Mwongozo naMafunzo kwa Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji wadogo wa madiniTanzania (FEMATA), mwongozo huo unaoelezea namna bora ya uchukuaji wa sampuliza uchunguzi wa kimaabara pamoja na namna bora ya kufanya uchenjuaji madini.
Aidha, Waziriameeleza kuwa, kwa kipindi kirefu GST imekuwa ikifanya kazi zake za kitaalamuna wachimbaji wadogo kwa kuwapa elimu ya kitaalam kwa kutumia machapishombalimbali kama vile Vipeperushi, vitabu pamoja na kuwatembelea katikamaeneo ya uchimbaji kwa lengo la kuwaelimisha wachimbaji wadogo juu yautafutaji na uchimbaji bora wa madini, kwa kufanya hivyo GST kupitiatafiti za awali imekuwa kichocheo kikubwa cha ukuaji wa Sekta Madini nchini kwakuzingatia mchango wake mkubwa katika pato la taifa ambao umefikia asilimia5.2 kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020.
“Ndugu zanguwachimbaji, Madini ni sayansi hivyo ni vyema kutumia mafunzo haya ili kujifunzanamna bora ya kutafuta, kuchimba na kuchenjua madini kwa kufuata maelekezo yakisayansi kwa kufanya hivyo mtatatua changamoto ya kuchukua sampuli na kufanyauchimbaji wa madini ulio na tija kiuchumi na kuleta maendeleo zaidi katikasekta hii kwa sababu mchimbaji atachimba bila kupoteza muda au mtaji” Bitekoalisisitiza.
Kwa upande wake,Mtendaji Mkuu wa GST Dkt. Mussa Budeba, alisema kuwa GST ilibaini uwepo wachangamoto ya uchukuaji sampuli za miamba zisizo zingatia taratibu zaubora kwa ajili ya uchunguzi wa maabara, kwa kutambua hilo GST imeamua kuandaakitabu cha Mwongozo na Mafunzo ya siku mbili kwa Viongozi wa FEMATA juu yanamna bora ya uchukuaji sampuli za uchunguzi na uchenjuaji madini.
Akielezea kuhusumwongozo huo, Dkt. Budeba alifafanua kuwa uchukuaji wa sampuli ndio nguzo kuuya uchimbaji wa uhakika kwa kupitia mwongozo huu utawawezesha wachimbaji wadogowengi kuwa na uwezo wa kutambua Mbale zenye uzalishaji mdogo, wa kati na wakiwango cha juu hii itawawezesha kufanya kazi kwa kujiamini, kuongezauzalishaji na kuokoa muda.
Uzinduzi wa Mwongozona Mafunzo kwa Viongozi wa FEMATA yameudhuriwa na viongozi mbalimbali kutokaWizara ya Madini akiwemo Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya, KatibuMkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila, GST, Tume ya Madini pamoja naViongozi na Wachimbaji wa FEMATA kutoka mikoa mbalimbali nchini.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.