Na:Sofia Remmi.
Habari:DodomaRs
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ametoa wito kwa wananchi wote waliojiandikisha katika daftari la wapiga kura kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura ili kutimiza haki yao ya kikatiba.
Akizungumza wakati akifungua kikao kazi chake na Wadau wa Ushirika Mhe. Senyamule alisema uzoefu unaonyesha kuwa wananchi wengi wanajiandikisha lakini hawajitokezi kupiga kura.
Amesema kwa mwaka 2020 Mkoa wa Dodoma ulikuwa na takwimu mbaya ambapo katika zoezi la uandikishaji ulifanya vizuri kwani asilimia 94 walijiandikisha na kupewa vitambulisho vya kupigia kura,lakini ni asilimia 45 tu ndio waliojitokeza kupiga kura.
“Hadi hivi sasa Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) imeshafanya kazi yake vizuri, sasa kazi kubwa imebaki kwetu kuhakikisha tunahamasisha makundi yote yaliyojiandikisha kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kutimiza haki yao ya kikatiba. Kazi iliyopo na tunayoendelea nayo ni kufanya asilimia 100 ya waliojiandikisha kujitokeza kupiga kura''amesema Mhe. Senyamule.
Katika hatua nyingine Mhe. Senyamule alisema Rais Dk.Samia amefanya kazi kubwa kuhakikisha Ushirika unaendelea kustawi na kunufaisha wakulima wengi,ambapo alitoa fedha kwa ajili kuhakikisha Benki ya Ushirika inaanzishwa” Aliongeza Mhe. Senyamule.
Kwa upande wake Mkulima kutoka wilaya ya Bahi Maxmiliani alisema Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia imetoa sh.bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa skimu ya umwagiliaji.
Akizungumza kuhusu uchaguzi Mkuu 2025, alisema wapo tayari kushiriki kwani ni haki ya kikatiba,vilevile kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya kilimo na Taifa kwa ujumla.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.