Na; Happiness E. Chindiye
Habari - Dodoma RS
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Khatibu Kazungu, ameendelea na ziara yake ya kujitambulisha katika Halmashauri za Bahi na Chemba.
Akizungumza na Viongozi pamoja na Watumishi wa Serikali katika Halmashauri hizo, Dkt. Kazungu amewaelekeza Wakurugenzi kutenga maeneo yatakayowawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika kilimo ili kuongeza kipato cha mkoa na kutoa ajira.
“Mkoa wetu wa Dodoma ndiyo Makao Makuu ya Nchi, hivyo ni vyema wananchi wawe na kipato cha uhakika ili kujikimu na familia zao. Sisi kama viongozi ni lazima tubuni mbinu hasa katika sekta ya uzalishaji,” alisema Dkt. Kazungu.
Aidha, aliwataka Watumishi kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu za Utumishi wa Umma sambamba na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, na kuitafsiri dira hiyo kwa vitendo ili kufanikisha malengo yake.
Vilevile, aliwataka viongozi wa Halmashauri hizo kuhakikisha watumishi wanapata haki zao za msingi ikiwemo likizo, uhamisho, malipo ya posho pamoja na kuimarisha mahusiano mazuri kazini.
Akihitimisha, Katibu Tawala huyo aliwakumbusha watumishi hao kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la upigaji kura Oktoba 29, 2025.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.