UJUMBE wa watu 41 wakiwemo Madiwani na wataalam wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela iliyopo Mkoani Mwanza umeanza ziara ya siku mbili katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma jana Oktoba 8, 2018 kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa mambo mbalimbali katika uendeshaji wa Halmashuri.
Ujumbe huo unaoongozwa na Mstahiki Meya wa Halmashauri hiyo Mhe. Renatus Mulunga, pamoja na mambo mengine, umelenga kupata uzoefu zaidi katika nyanja za ukusanyaji wa mapato, usafi wa Mazingira na udhibiti wa taka ngumu , pamoja na Mipango Miji.
Ziara hiyo pia itahusisha utembeleaji wa miradi ya kimkakati ikiwemo Stendi Kuu ya kisasa ya mabasi na Soko Kuu la kisasa katika eneo la Nzuguni, ukanda wa Uwekezaji Njedengwa, na dampo la kisasa la kuhifadhia taka lililopo eneo la Chidaya.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Godwin Kunambi akizungumza wakati wa ziara ya Madiwani na Wataalam wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela iliyopo Mkoani Mwanza walipotembelea Jiji la Dodoma Oktoba 8, 2018.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.