MADIWANI wa Halmashauri ya jiji la Dodoma wametakiwa kuwasilisha changamoto zinazohitaji utatuzi wa haraka ili ziweze kushughulikiwa mapema na kuwahakikishia wananchi huduma bora.
Kauli hiyo ilitolewa na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya jiji la Dodoma Mhe. Prof. Davis Mwamfupe alipokuwa akifunga mkutano wa kawaida wa baraza la madiwani uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya jiji la Dodoma jana.
“Wameshimiwa madiwani shida inapotokea, tupewe taarifa mapema ili itatuliwe mara moja, tusisubiri vikao vya Baraza kwa sababu vikao hivi ni vya maamuzi lakini vipo vikao vya kiutendaji ambavyo hufanyika mara kwa mara vitumike kutatua changamoto zinazohitaji utatuzi wa haraka".
Mstahiki Meya huyo alilikumbusha Baraza hilo kuwa Madiwani ndiyo jicho la wananchi, na kuwataka kufuatilia kama fedha zinazotolewa na Halmashauri zinafika kwa wakati na kufanya kazi iliyokusudiwa katika maeneo yao huku akisisitiza umuhimu wa taarifa juu ya matumizi bora ya fedha zilizokusanywa kuwa utasaidia kuondoa mkanganyiko kwa wananchi na kuondoa upotoshaji unaoweza kufanyika au kujitokeza.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.