Na Ramadhani Juma
OFISI YA MKURUGENZI
MADIWANI wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma wameelezea kufurahishwa kwao na agizo alilotoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dokta John Pombe Magufuli kuhusu kuundwa kwa timu itakayokuwa na kujumu la kufanya utafiti na kuishauri Serikali endapo kuna haja ya kuendelea kuwa na Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao Makuu (CDA) katika kuendeleza mji wa Dodoma au jukumu hilo lifanywe na Halmashauri ya Manispaa kama ilivyo katika Manispaa zote nchini.
Wakichangia taarifa ya Katibu wa Baraza la Madiwani la Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi ambaye pia ndiye Mkurugenzi wa Manispaa hiyo jana, wajumbe wa Baraza hilo walidai kuwa sasa imefikia wakati Mamlaka hiyo uvunjwe kwani imekuwa ikisababisha migogoro mingi ya ardhi badala ya kuupanga Mji huo kwani ndio jukumu lao la msingi.
Madiwani wote waliopata fursa ya kuchangia taarifa hiyo walieleza kuwa, wananchi wa Manispaa ya Dodoma wamechoshwa na uwepo wa Mamlaka ya CDA na kwamba imewanyanyasa kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na kuwapora ardhi zao bila kuzingatia sheria na taratibu.
Hivi karibuni Mheshimiwa Rais Dokta John Magufuli akiwa Mjini Dodoma aliagiza pamoja na mambo mengine, kufanywa majadiliano kati ya wadau ambao ni uongozi wa Mkoa, Mamlaka ya Ustawishaji (CDA), Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, Wizara ya Ardhi na mamlaka zote zinazohusika ili ziiishauri Serikali juu ya umuhimu wa kuendelea au kutoendelea na Mamlaka ya hiyo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.