Na. Dennis Gondwe, DODOMA
MADIWANI na wataalam wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametakiwa kuwahimiza wananchi katika kata na mitaa kulipa kodi kwa hiari ili waweze kujiletea maendeleo.
Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Asma Karama katika mkutano wa Baraza la Madiwani kupitia na kujadili rasimu ya mapendelezo ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Karama alisema “ndugu zangu, tuendelee kukusanya mapato kwa wingi, maana yake matumizi bila mapato haiwezekani. Kwa pamoja tukawahamasishe wananchi wetu kwenye kata na mitaaa waweze kulipa kodi bila shuruti ili tuweze kupata mapato na kuwaletea maendeleo yao”.
Aidha, aliishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa kurudisha vyanzo vingine vya mapato kwenye halmashauri. Alisema kuwa kurudishwa kwa vyanzo hivyo zitaiwezesha halmashauri kutoa huduma za afya, elimu na jamii kwa ujumla.
Vilevile, alipongeza kwa maandalizi ya rasimu ya bajeti na kuyaita kuwa ni mazuri. “Napenda kumshukuru Mstahiki Meya, madiwani, Mkurugenzi wa Jiji na wataalam wote kwa kazi nzuri mliyoifanya ya kuchakata bajeti hii na kuwa bajeti bora itakayotuvusha mwaka wa fedha 2024/2025” alisema Karama.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.