MKUU wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge amewataka Madiwani Wanawake kusimamia Halmashauri katika utekelezaji wa miradi ya Afya, Elimu Miundombinu, Biashara pamoja na huduma za kijamii ili miradi iweze kukamilika kwa wakati.
Agizo hilo amelitoa Mei 5,2021 jijini Dodoma wakati akifunga mafunzo ya kuwawezesha Madiwani wanawake kutoka Halmashauri za jiji la Dodoma,Chamwino na Chemba yaliyofanyika kwa siku tatu na kufadhiliwa na Shirika la Hanns Seidel Foundation (HSF) Tanzania na Uganda.
Dkt.Mahenge amesema kuwa lazima mkazingatie viwango vyote vya ubora viendane na thamani halisi ya fedha katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye ngazi ya Halmshauri/Serikali za Mitaa.
”Nimeambiwa kuwa mafunzo haya yamehudhuriwa na washiriki 40 nawapongeza kwa kwa kujitokeza kushiriki mafunzo hayo nawaomba mliyojifunza hamtayaacha hapa bali mtayaweka katika matendo yenu ya kila siku”amesema Dkt.Mahenge
Aidha Dkt.Mahenge amewataka kusimamia sula la ukusanyaji mapato (mapato ya ndani) pamoja na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato na kuzuia ubadhirifu wa fedha za Serikali unaofanywa kwa njia mbalimbali.
”Mafunzo haya yakawe chachu katika kusimamia Halmashauri zenu katika uendeshaji wake,matumizi ya fedha kwa kufuata taratibu na kusimamia kanuni za kisheri ili kuondokana na hoja za CAG na kuepukana na kupata hati chafu na zenye mashaka”amesisitiza
Amesema kuwa tayari ripoti ya CAG imeshatoka kwenye Halmashauri zetu kupitia hoja zote zilizoibuliwa na kuziwekea mkakati wa kuzishughulikia na kuzimaliza zote.
Hata hivyo amesema kuwa amefarijika kuona kwamba mafunzo haya ya siku tatu yamegusa wanawake zaidi,imani yangu kuwa kutakuwa na ongezeko la wanawake watakaoteuliwa,kuchaguliwa na kushiriki katika siasa ndani na nje ya vyama vya siasa.
”Hili ni muhimu zaidi katika ukanda wetu huu ambapo kushamiri kwa mfumo dume kumechangia kupungua kwa idadi ya wanawake wanaoshiriki katika shughuli za kisiasa na kiungozi”amesema Dkt.Mahenge
Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum ambaye amewezesha uwepo wa mafunzo hayo kwa kuomba Ufadhili kwenye shirika la HSF Mhe.Fatma Toufiq amesema kuwa sababu ya kuwaita madiwani wanawake ni kuwafundisha masuala mbalimbali ili waweze kutenda kazi zao kwa weledi.
”Kuna masuala mbalimbali wamejifunza hapa kanuni,Diwani anatakiwa awaje,kufatilia msuala mbalimbali ya bajeti maana tumetoka kwenye uchaguzi hivyo kuna madiwani wapya lazima waweze kujua jinsi gani ya kuwatetea wanawake katika jamaii inayowazunguka”amesema Mhe.Toufiq
Katika mkutano huu kulikuwa na madiwani 40 lakini miongoni mw madiwanai hao ni wa vitu maalum pamoja na madiwani wa kata,tunajua madiwani wa kata kazi zao ni kusimamia katika kata pamoja na vijiji vinavyowazunguka lakini wa viti maalum wao wanasimamia tarafa.
”Tunaamini mafunzo hayo yawasaidia kufanya kazi kwa weledi pamoja na nakuona bajeti katika halmashauri zao na kushirika masula mbalimbali ili waweze kuishauri vizuri Serikali hatimaye maendeleo endelevu yaweze kupatikana”amesisitiza Mhe.Toufiq
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.