MADIWANI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametakiwa kuwasilisha taarifa za changamoto mapema ili ziweze kutatuliwa na halmashauri badala ya kusubiri vikao.
Kauli hiyo ilitolewa na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe alipokuwa akifunga mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Prof. Mwamfupe alisema kuwa madiwani wanapokumbana na changamoto zinazohusiana na utekelezaji wa shughuli za maendeleo wasisubiri vikao. “Karibu asilimia 75 ya hoja tulizojadili zinategemea kuwasilisha taarifa za changamoto tofauti na kusubiri vikao” alisema Prof. Mwamfupe.
Akimkaribisha Mwenyekiti kufunga mkutano wa Baraza la Madiwani, katibu, Wakili Msekeni Mkufya aliwataka madiwani kuendelea kushirikiana na wataalam wa halmashauri katika kuleta maendeleo ya halmashauri. “Wito wangu kwenu, tuendelee kushirikiana kwa sababu wote tunajenga nyumba moja, kwa maana ya kuwahudumia wananchi” alisema Wakili Mkufya.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.