MKURUGENZI Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, SACF. James John, aliwataka madiwani hao kujifunza namna mbalimbali za kukusanya mapato kupitia ziara hiyo waliyoifanya ili kukuza uchumi wa Kyerwa. “Kwanini nilitamani tuje Dodoma, ni kwamba, kuamua ni bora sana kuliko kusitasita, lakini kuamua kwa manufaa ya taasisi, kwamba leo sisi tunafanya haya maamuzi makubwa watu hawatatuelewa, watatulaumu lakini kokote tutakakokuwa miaka ya mbeleni tutasema wakati sisi tuko kwenye halmashauri tulifanya moja na mbili. Kwahiyo, jambo ambalo natamani tuondoke nalo hapa ni kuthubutu kufanya bila kujali ‘size’ ya kipato chetu” alisema SACF. John.
Vilevile, Diwani wa Kata ya Matunguru, Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, Florence Frederick, aliipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma, kwa kuonesha uthubutu katika kuanzisha na kuendeleza miradi. “Nimejifunza mambo mengi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, kupitia ziara hii, mfano Shule ya Dodoma English Medium School. Kwahiyo, tumejifunza na sisi tutaenda kufanya juhudi zetu tuwe na shule nzuri kama hiyo. Naipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma, kwa mipango yake mizuri na mapato wanayopata, inaonekana walithubutu na sisi tutathubutu ili mambo yaende vizuri” alipongeza Frederick.
Madiwani hao waliwasili Halmashauri ya Jiji la Dodoma tarehe 17 Desemba, 2024 kwa ajili ya ziara ya siku moja, yenye lengo la kutembelea miradi ya kimkakati iliyopo jijini Dodoma na kujifunza uthubutu wa kufanya mambo mbalimbali ya kimaendeleo ili kuongeza mapato ya Halmashauri yao
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.