• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Maelfu wamiminika kutaka kitambulisho cha Taifa

Imewekwa tarehe: January 16th, 2020

ZIKIWA siku zinayoyoma kufikia siku ya ukomo (20/01/2020) wa usajili wa laini za simu kwa kutumia namba za kitambulisho cha Taifa, kitambulisho hicho kimeonekana kuwa lulu, lakini mbali na usajili wa simu usipokuwa na kitambulisho cha taifa utakutana na ugumu katika katika kukamilisha mambo 10 siku za usoni.

Mateso wanayoyapata wananchi wasiokuwa na vitambulisho hivyo kwa sasa katika kuvifukuzia inatokana na kutaka kwao kuwahi kusajili laini za simu kwa njia ya alama za vidole.

Mwamko wa kutafuta kitambulisho cha Taifa umeonekana zaidi mwaka 2019 na Januari 2020, baada ya Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) kutangaza kuzima simu ambazo hazijasaliwa kwa alama za vidole.

Kwa mujibu wa TCRA hadi Januari 12, mwaka huu laini za simu milioni 26 ndizo zilizokuwa zimesajiliwa kati ya 48 milioni.

Ili uweze kusajili laini yako kwa mfumo wa alama za vidole, ni lazima uwe na kitambulisho cha Taifa au namba za kitambulisho hicho.

Upatikanaji wa kitambulisho hicho hupitia mchakato mrefu ikiwemo kuwasilisha vithibitisho vya uraia kama vyeti vya kuzaliwa au viapo ambavyo ni lazima vithibitishwe na Idara ya Uhamiaji.

Ingawa kwa sasa umuhimu wake unaonekana zaidi katika usajili wa simu, lakini ukweli ni kuwa unaweza kukutana na mateso siku za usoni utakapohitaji huduma nyingine katika taasisi mbalimbali kama huna kitambulisho hicho.

Unayoweza kukwama kwa kukosa kitambulisho hicho

Moja ya changamoto unayoweza kukutana nayo ni wakati utakapohitaji pasi ya kusafiria ya kielektroniki ambayo bila kuwa na kitambulisho cha Taifa huwezi kuipata, hii itakufanya ushindwe kusafiri.

Nyingine ni unapotafuta ajira serikalini, kusajili kampuni kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brella) na unapotafuta leseni ya udereva Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Pia kitambulisho cha Taifa kitahitajika katika kutafuta leseni ya biashara, hati ya makazi, hati ya kiwanja, kumdhamini mtu polisi, mahakamani na unapotaka kuingia kwenye mifuko ya hifadhi za jamii.

Baadaye kuna mipango ya kuunganisha kanzi data ya NIDA na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ili itumike katika kuhuisha daftari la wapiga kura ili kitambulisho hicho kitumike kupigia kura.

Mkurugenzi wa Leopard Hoteli ya mjini Moshi, Priscus Tarimo akizungumzia umuhimu wa kitambulisho hicho alisema kina faida nyingi ikiwamo kumtambulisha mtu halisi na kuepukana na matapeli.

“Lakini kitambulisho hiki ni muhimu wakati wa kutafuta `passport (pasi ya kusafiria), kuziba mianya ya ukwepaji kodi na kuongeza mapato, kuondoa udanganyifu wa umri na kudhibiti uhalifu,” alisema.

Mkazi wa jijini Dar es Salaam, Ally Janja alisema kitambulisho hicho ni muhimu kwani ndicho kinachoonyesha utaifa wa mtu na pia kudhibiti uhalifu kitaifa na kimataifa.

Samson Mollel, mjasiriamali katika stendi kuu ya mabasi jijini Arusha alisema kitambulisho cha Taifa ni muhimu kwani kitasaidia kuwatambua Watanzania na wasio Watanzania na kudhibiti uhalifu.

“Mimi ni mhanga wa wizi wa mtandaoni na nilipokwenda polisi kumfuatilia mhusika hatukufanikiwa kwa sababu kitambulisho alichosajili nacho kilikuwa ni cha bandia. Hiki cha NIDA ni baba lao,” alisema.

Wakili wa kujitegemea, Peter Mshikilwa alisema kitambulisho cha Taifa ndio uraia na kwamba kina faida nyingi na sasa kimekuwa ni muhimu hata katika kupata huduma katika taasisi za umma.

Mshikilwa alisema hata kwa mtu anayetaka kusajili kampuni Brella ni lazima awe na kitambulisho cha Taifa vinginevyo kampuni haiwezi kusajiliwa akiongeza hilo litasaidia kuwajua wanahisa halisi.

Wakazi wa Jiji la Dodoma wakiwa katika foleni ya kufuatilia vitambulisho vya taifa katika ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) jijini Dodoma.


Chanzo:Gazeti la Mwananchi


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.