Na. Dennis Gondwe, DODOMA
MAENDELEO ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma yanategemea utayari wa wananchi kulipa kodi za serikali kwa hiari na kuwa sehemu ya mchakato wa maendeleo.
Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo katika mahojiano maalum yaliyofanyika ofisini kwake jijini Dodoma.
Fungo alisema kuwa yanapoongelewa maendeleo ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma hayawezi kutenganishwa na kodi zinazolipwa na wananchi. “Niwaombe wananchi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, kulipa kodi kwa hiari. Jiji la Dodoma ni letu sote. Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imefanya mambo makubwa kwenye nchi yetu. Fedha nyingi zimeletwa katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo. Fedha nyingi zimeletwa kugharamia miradi ya shule, kugharamia vituo vya afya na kugharamia miundombinu katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma” alisema Fungo.
Aidha, aliwaomba wananchi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kulipa kodi kwa hiari. “Ndugu zangu fedha hizo zinazoletwa na serikali ndiyo kodi tunayolipa. Hebu tuwe na moyo wa kizalendo kulipa kodi kwa mujibu wa sheria. Tulipe Kodi za ardhi, ushuru wa huduma na hoteli na kodi zote zilizopo kwa mujibu wa sheria. Tuzilipe hizi kodi ndizo zinatusaidia kufanya maendeleo makubwa katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Huku ndiko kuunga mkono juhudi za Rais wetu za kuleta maendeleo” alisema Fungo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.