IMEELEZWA kuwa mbinu muhimu za kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza ni pamoja na kubadili mtindo wa maisha kwa kudhibiti matumizi ya vilevi kama sigara na pombe, matumizi ya sukari na chumvi, kufanya mazoezi ya mwili pamoja na kuepuka tabia bwete.
Akifungua Kongamano la nne la Kisayansi katika wiki ya maadhimisho ya wiki ya Magonjwa Yasiuoambukiza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe amesema Serikali inaendelea kuboresha miundombinu na kununua vifaa tiba vya kisasa vikiwemo vifaa vya uchunguzi vinavyowezesha wanasayansi kufanya kazi zao kiurahisi ili kugundua magonjwa mapema hususan yasiyoambukiza.
"Kwa sasa tumeshuhudia maboresho yaliyofanyika katika Taasisi zetu za Ocean Road, NIMR, JKCI, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Hospitali za Kanda, Hospitali za Mikoa, Wilaya hadi Zahanati pamoja na Hospitali binafsi." Amesema Prof. Mdoe
Huduma za Uchunguzi na utambuzi wa magonjwa (Maabara), Mionzi na Radiolojia zimeboreshwa kwa maana ya miundombinu na vifaa vya kisasa ili kurahisisha utoaji huduma ya magonjwa yasiyoambukiza na uwezo wa kufanya tafiti mbambali za kisayansi.
Aidha, Prof. Mdoe ametoa wito kwa taasisi kujiwekeza katika kutoa huduma, waongeze kasi pia ya kufanya tafiti za kisayansi zitakazowezesha wananchi kujikinga na magonjwa haya na pia kutoa mbinu mpya za matibabu zitakazowezesha
Pia, amewataka wataalamu hao kujadiliana juu ya matumizi ya dawa za asili ambazo nyingine zimekuwa zikitumika kutibu Pumu, Shinikizo la juu la damu na Saratani.
"Tuweke mfumo sahihi wa kuwezesha dawa hizi za asili zikithibitika kisayansi kuwa zinatibu na hazina madhara ili tuweze kuzitumia kudhibiti magonjwa haya yasiyoambukiza." Amesema Prof. Mdoe
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan inaendelea kufanya kazi na wadau wote wenye nia ya kusaidia mapambano dhidi ya magonjwa Yasiyoambukiza, kwani bila
kufanya hivyo mlipuko wa magonjwa haya utaendelea kuua watu wengi, kuleta ulemavu na mwisho kurudisha nyuma jitihada za Taifa kukuza uchumi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.