MGOMBEA wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli leo amepokea Cheti cha Ushindi wa Kiti cha Urais kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage mara baada ya kutangazwa mshindi wa kiti hicho katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, hafla hiyo ya kukabidhiwa Cheti imefanyika katika Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma leo tarehe 01 Novemba 2020.
Hayo yamejiri leo Jijini Dodoma ambapo Dkt. Magufuli ambaye ni maarufu kwa uchapakazi wake wenye matokeo makubwa amewashukuru Watanzania huku akiwakumbusha Watanzania kuendelea kuchapa kazi.
Dkt. Magufuli amewashukuru Watanzania kwa kukipatia ushindi chama chake cha Mapinduzi (CCM) katika nafasi ya Urais, Ubunge, Udiwani na kule Zanzibar katika nafasi ya Urais, Uwakilishi na nafasi ya Udiwani.
''Kupata asilimia 84.4 ni imani kubwa sana kwa Watanzania na nasema kwa dhati nina deni kubwa sana kwa Watanzania, imani yao nitaitimiza kwa kufanya kazi sana usiku na mchana,
Siasa sio vita siasa sio ugomvi sisi sote ni Watanzania napenda kuwaahidi nitashirikiana nanyi katika kuhakikisha tunasukuma mbele gurudumu la maendeleo ya nchi yetu. Tanzania kwanza mambo mengine baadae". Amesema Rais Mteule Dkt. Magufuli..
Aidha, Magufuli amewashukuru wapinzani wake waliokubali matokeo akisema ''Nawashukuru na kuwapongeza kwa kukubali matokeo na kuja kushiriki hafla hii. Hii ni ishara ya kukomaa kwenu kisiasa hongereni sana. Ni kweli kwamba wananchi wametupatia ushindi mkubwa sana, lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya kudharau maoni na ushauri wenu" alizidi kubainisha Rais huyo mteule.
Vile vile aliendelea kutoa shukurani zake kwa kusema "Navishukuru pia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwa kufanya kazi kwa weledi mkubwa na kuhakikisha amani na usalama vinatawala katika kipindi chote cha uchaguzi,'' alisema kiongozi huyo.
Rais Mteule Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuapishwa Novemba 5, 2020 Jijini Dodoma katika uwanja wa Jamhuri.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Cheti cha Ushindi wa Kiti cha Urais kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage mara baada ya kutangazwa mshindi kwa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, hafla hiyo ya kukabidhiwa Cheti imefanyika katika Makao Makuu ya Tume ya Uchaguzi NEC Njedengwa jijini Dodoma leo tarehe 01 Novemba 2020.
Makamuwa Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Cheti cha Ushindi wa Kiti chaMakamu wa Rais kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) JajiMstaafu Semistocles Kaijage.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akionesha Cheti cha Ushindi wa Kiti cha Urais alichokabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage mara baada ya kutangazwa mshindi kwa Kiti cha Urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama na Waliogombea Urais kupitia vyama Mbalimbali vya Upinzani nchini wakati Wimbo wa Taifa ukipigwa katika hafla fupi ya kukabidhi Cheti cha Ushindi kwa Kiti cha Urais zilizofanyika katika Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Njedengwa jijini Dodoma leo tarehe 01 Novemba 2020.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.