SEKSHENI ya Elimu Mkoa wa Dodoma imeendelea na ziara ya kukagua maendeleo ya mahudhurio ya wanafunzi kwa muhula mpya wa masomo ulioanza jana Januari 8, 2024 ambapo leo Afisa Elimu Mkoa Mwl . Vicent Kayombo ametembelea shule ya Msingi Mazengo iliyopo kata ya Kikuyu pamoja na shule ya sekondari Kiwanja cha ndege zote zikipatikana Jijini Dodoma.
Ziara hiyo ya kukagua Mahudhurio ya wanafunzi pamoja na Maendeleo ya masomo ya kozi ya kiingereza kwa kidato cha kwanza imebaini kuwa mahudhurio pamoja na masomo hayo yanaridhisha.
Mbali na hilo, Afisa Elimu huyo amefanya kikao cha pamoja na Walimu wa shule zote zilizopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwenye ukumbi wa shule ya Msingi Umonga kikiwa na lengo la kubainisha changamoto za walimu pamoja na kutoa mwongozo juu ya mipango na mikakati ya mkoa kwa mwaka 2024.
Aidha Mwl. Kayombo amewasihi walimu wote kuwa na umoja na mshikamano kati yao ili kujenga urafiki katika kazi na kuwataka kuacha kuwatishia wanafunzi katika masomo hususani wale ambao wanaanza kwa mara ya kwanza (kidato Cha kwanza) na kuwasihi kutumia mbinu za ufundishaji zile walizojifunza wakiwa masomoni ili kuwafanya wanafunzi waweze kuelewa haraka.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.