WAZIRI Mkuu amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi na Mkurugenzi wa mwenzake wa Chamwino kuhakikisha vijana wengi wanapata fursa za ajira kwenye mradi wa ujenzi ofisi za serikali.
Majaliwa ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi za Wizara na ofisi ya Mwanasheria mkuu wa Serikali eneo la Mtumba lililopo kilometa 17 kutoka katikati ya Jiji la Dodoma.
"Mkurugenzi wa Jiji wasiliana na Mkurugenzi mwenzako wa Chamwino mhakikishe vijana na akina mama wanakuja kufanya kazi hapa. Pia itisha kikao cha waandishi wa habari uwaeleze wananchi wako fursa zilizopo, kuanzia ufyatuaji wa matofali, uuzaji wa nondo, kokoto na utengenezaji wa 'pavement blocks' hizi zote ni fursa, tuna wizara 24 na mahitaji ni makubwa" alisisitiza.
Mapema akitoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Bwana Anthony Mavunde alisema zoezi la kusafisha eneo la ujenzi wa mji wa Serikali lilianza Novemba 28 mwaka huu.
Alisema wizara zote zimepata viwanja na zimeanza ujenzi isipokuwa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana) ambao bado wanasubiri kupatiwa fedha. Aidha, alisema kuwa kazi ya ujenzi wa Mji wa Serikali inasimamiwa na Kamati ya Kitaifa ya kuratibu zoezi la Serikali kuhamia Dodoma, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma.
Waziri Mkuu akikagua maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi za Wizara mbali mbali kwenye eneo la Mji Mkuu wa Serikali
Waziri Mkuu akipewa maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi kutoka kwa mhandisi wa mkandarasi wa ujenzi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.