Angela Msimbira ARUSHA
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameiagiza Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha kukamilisha utaratibu mpya wa usimamizi wa utoaji wa mikopo inayotokana na asilimia 10 ya Mapato ya ndani ya Mamlaka za Serikali za Mitaa ifikapo januari 15, 2024.
Maelekezo hayo ameyatoa Novemba 22,2023 alipokuwa akifungua maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Kifedha Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Alisema ukamilishaji wa taratibu za usimamizi wa utoaji wa mikopo utazisaidia Halmashauri kutoa mikopo hiyo kwa wananchi karibu na maeneo wanayoishi huku akiagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanaendelea kuratibu vikundi vyote vya wajasiriamali, kuwatafutia maeneo ya kufanyia biashara zao na kubuni maonesho ya ndani ya Wilaya na Mikoa ili watumie fursa hiyo kutangaza bidhaa zao.
"Serikali ilisitisha utoaji wa mikopo ya asilimia 10 tangu mwezi Aprili, 2023 ni matumaini yangu kuwa fedha hizo zipo katika Halmashauri na wanufaika watapata mikopo kwa wakati” alisisitiza Mhe. Majaliwa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.