WAZIRI MKUU Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amekagua ujenzi wa mradi wa kitega uchumi unaotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika Mji wa Serikali Mtumba ikiwa ni sehemu ya matukio ya kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania.
Akizungumza baada ya kukagua ujenzi huo, Mheshimiwa Majaliwa amelipongeza Jiji la Dodoma kwa kutekeleza mradi huo na kuyataka majiji mengine nchini kuiga mfano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Mradi huo unajengwa kwa awamu mbili na utagharimu shilingi bilioni 59.3. Mradi huo unajumuisha jengo la hotel, maduka na huduma za kibenki, kumbi za mikutano ikiwemo ukumbi mkubwa wenye uwezo wa kuhudumia washiriki 1,000 kwa wakati mmoja na kumbi ndogo 6 zenye uwezo wa kuhudumia washiriki 120 kwa wakati mmoja.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alipokuwa akikagua mradi wa kitega uchumi unaotekelezwa na Halmashsuri ya Jiji la Dodoma ndani ya eneo la Mji wa Serikali.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa nasaha zake mara baada ya ukaguzi wa mradi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika Mji wa Serikali ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.