WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezitaka Halmashauri nchini kuongeza umakini katika manunuzi ya vifaa vinavyotumika katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao ili iweze kukamilika katika muda uliopangwa na kutoa huduma kwa wananchi.
Ametoa wito huo leo (Jumanne, Novemba 29, 2022) alipozungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Kisarawe, Mkoani Pwani.
Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Wenyeviti wa Halmashauri wanapaswa kuwa wakali katika kufuatilia manunuzi ya vifaa mbalimbali na watumie wakaguzi wa ndani katika kufuatilia taarifa za manunuzi.
“Manunuzi hapa kisarawe ni ya gharama kubwa katika miradi yenu, miradi haishi kwasababu ya gharama kubwa, na bahati mbaya mnafanya hivyo kwa fedha za Serikali kuu”
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ameiagiza Taasisi ya Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kumfuatilia aliyekuwa afisa mapato katika Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe Fredy Bandai aliyehamishiwa Mtwara vijijini “Huyu asimamishwe kazi na arejeshwe Kisarawe ili aje atolee taarifa ya fedha kiasi cha shilingi milioni 253 alizokusanya lakini hazionekani”
Pia, Waziri Mkuu amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kisarawe James Chitumbi kwa kukiuka maadilin ya uongozi.
Kadhalika Waziri Mkuu amewataka wakuu wa Idara kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yao “Tunataka watanzania wahudumiwe, ninyi watumishi wa umma ni wahudumu kwa wananchi wetu, fuatilieni miradi ili iweze kuleta tija kwa wananchi”.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.