WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na maendeleo na kasi ya ujenzi wa mabehewa mapya kwa ajili ya Reli ya Kisasa (SGR) ya Shirika la Reli la Tanzania yanayotengenezwa na kampuni ya Sung Shin Rolling Stock (SSRT) iliyoko nchini Korea Kusini.
“Kati ya mabehewa 81 ambayo Tanzania inatengeneza kutoka kwenu, tayari 36 yamekamilika na yameshapelekwa nchini Tanzania na 45 yaliyobaki yanategemewa kukamilika Machi, 2023. Mabehewa haya ni ya daraja la tatu na yatatoa huduma zote muhimu.”
Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo jana Oktoba 24, 2022 mara baada ya kutembelea kampuni ya SSRST inyotengeneza mabehewa na injini za treni nchini Korea Kusini.
Kadhalika, Waziri Mkuu amemkaribisha nchini Rais wa Kampuni hiyo Gye Shul Park aje kuwekeza nchini Tanzania kutokana na fursa mbalimbali zilizopo ikiwemo mpango wa Serikali wa kuendelea kuiboresha sekta ya usafiri wa reli.
“Mnakiwanda kikubwa, teknolojia ya hali ya juu pamoja na utaalam na wataalam kwenye eneo hili. Kwa sasa tuna mipango mikubwa ya kuendelea kuiboresha sekta hii ya usafiri wa reli, yapo maeneno tofauti kwenye mpango wa kuunganishwa na reli ya kisasa (SGR), nakukaribisha kuja kuwekeza kitu kama hiki Tanzania.”
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa alitembelea kituo cha Seamul Undong ambacho ni taswira ya maendeleo ya Korea kupitia mpango wa kuviwezesha vijiji ambao unatekeleza mpango huo nchini Tanzania katika mkoa wa Morogoro (Pangawe) na Zanzibar.
Mheshimiwa Majaliwa alimshukuru Rais wa Kituo hicho na kumuomba kuendelea kutoa ushirikiano ili kukuza zaidi mpango huo na kufikia maeneo mengi zaidi.
“Mfumo huu kwa sasa umekuwa wa kifaifa, ushirikishwaji wa Wananchi ni mkubwa. Sasa tunataka tuikuze zaidi, haya maeneo ya Morogoro na Zanzibar tunataka yawe mifano, kwenye utekelezaji wa eneo hili.”
Pia, Mheshimiwa Majaliwa alitembelea kituo cha ubunifu cha CEIC kilichopo katika mji wa Pangyo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.