WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku 15 kuanzia leo Oktoba 20, 2022 kwa kampuni ya Inter Country Contractors kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa miradi ya barabara katika kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza.
Mheshimiwa Majaliwa ametoa agizo hilo leo Alhamisi Oktoba 20, 2022 alipokutana na Waziri wa Nchi -OR TAMISEMI, Viongozi wa Wilaya ya Ukerewe na Watendaji wa TARURA ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma.
Waziri Mkuu amesema kuwa kampuni hiyo ilipewa kandarasi ya ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 13 kwa kiwango cha lami na changarawe katika kisiwa hicho ambapo ilipaswa kukamilisha kazi hiyo Julai 2022.
“Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan inatoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara, katika hili tumetoa kipaumbele kwa wakandarasi wazawa, tunachotegemea ni uaminifu wenu na utekelezaji wa miradi hii iwe ya viwango na mkamilishe kwa wakati”
Mheshimiwa Majaliwa amesema ni vyema Mameneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) Mikoa na Wilaya wakatekeleza majukumu yao ipasavyo ili kuhakikisha ujenzi wa barabara katika maeneo mbalimbali nchini na ukamilika kwa wakati na kwa viwango vilivyokusudiwa.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mheshimiwa Angellah Kairuki amesema wamepokea maelekezo ya Mheshimiwa Waziri Mkuu na kuahidi kufanya mapitio makubwa ya mfumo wa kiutendaji wa TARURA ili kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa miradi ndani ya taasisi hiyo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.