WAZIRI Mkuu Kasim Majaliwa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ana dhamira ya dhati kuhakikisha kila Mtanzania anapata fursa sawa ya kufanya biashara katika mazingira bora na Rafiki kwa biashara ili kukuza uchumi.
“Lengo la maboresho haya kwa wafanyabiashara wadogo ni kutaka kutengeneza fursa zaidi kwa kuwa na maeneo salama yanayotambulika na yanayoweza kutumika na taasisi za kifedha kutoa mikopo na fursa nyingine za kichumi.”
Waziri Mkuu ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Dodoma kwa ubunifu na kuwataka viongozi hao waendelee kusimamia mradi huo na kuukamilisha kwa wakati pamoja na kubuni maeneo mengine ya nje ya mji ili kukuza maeneo mengi zaidi kibiashara katika mkoa huo.
Aidha, Waziri Mkuu amewataka wafanyabiashara wadogo wa mkoa huo wafuate utaratibu utakaowekwa na mkoa huo mara baada ya ujenzi kukamilika. “Serikali imeendelea kutafuta fursa za kifedha kwa wafanyabiashara wadogo, hivyo jipangeni kutumia fursa hizo.”
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa amesema Mkmoa wa Dodoma umefanya kazi kubwa ya kutekeleza mradi rafiki kwa Wamachinga wa mkoa huo. “Niwasihi wakuu wa mikoa mingine kuiga mfano huu kwa kujenga miradi ya kuwapanga machinga kulingana na mazingira yaliyo katika mikoa yenu.”
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.