WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inaendelea kufanya tathmini ili kuhakikisha inazuia ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (COVID-19) isiweze kusambaa kwa kiasi kikubwa nchini.
Pia, Waziri Mkuu amevishukuru vyombo vya habari nchini kwa ushirikiano wanaoutoa kwa Serikali katika kuelimisha umma namna ya kujikinga na virusi vya Corona.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo Jumatatu, Machi 23, 2020 wakati akizungumza na Mawaziri na Makatibu Wakuu katika kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Hazina, Jijini Dodoma.
Imeelezwa kuwa kinga dhidi ya virusi vya Corona liwe ni jambo la kimkakati zaidi kuliko kusubiri kutibu, hivyo kwa sasa Serikali imeweka mkazo kwenye kuwahamasisha wananchi kujikinga na virusi hivyo. "Mawaziri hakikisheni katika kipindi hiki ziara za kwenda kukagua miradi zielekezwe kwa Wakurugenzi, ikibidi kwa Makatibu Wakuu, Mawaziri mnatakiwa mjikite katika kukinga Taifa na Corona".
Awali, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema katika kipindi cha saa 24 jumla ya watu 292,142 duaniani walibainika kuwa na virusi vya corona kati ayao watu 12,784 walifariki.
Pia, katika Bara la Afrika watu 736 walibainika kuwa na virusi vya corona na kati yake watu 20 walifariki katika kipindi cha saa 24.
Kwa Tanzania, Waziri Ummy alisema jumla ya wtu 12 walibainika kuwa na virusi vya corona tangu mgonjwa wa kwanza alivyogundulika nchini na kwamba wagonjwa wote hali zao ni nzuri na mmoja ampimwa zaidi ya mara mbili na kubainika kuwa hana virusi.
Baadhi ya Mawaziri na Makatibu Wakuu wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (hayupo pichani) katika Kikao Kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Hazina, Jijini Dodoma leo kuweka mikakati ya udhibiti wa kuenea kwa virusi vya Corona nchini.
Chanzo: dailynews_habarileo (instagram)
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.