Na. Dennis Gondwe, DODOMA
BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma limekubali kwa kauli moja maombi ya kuanzisha ushirikiano baina ya Jiji la Nagai la nchini Japan na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.
Akiwasilisha taarifa ya Mwenyekiti katika Mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani, Mwenyekiti wa mkutano huo ambae pia ni Mshahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe alisema kuwa siku kadhaa zilizopita ofisi yake ilitembelewa na Balozi wa Tanzania nchini Japan, Balozi Baraka Luvanda na kuwasilisha barua ya kuomba ushirikiano huo. “Madhumuni ya kuwasilisha taarifa hii ni kuomba ridhaa ya Baraza la Madiwani kuanza mazungumzo ya makubaliano ya ushirikiano huo. Aidha, tayari Jiji hilo limeonesha utayari wa kutoa gari la kubeba wagonjwa na gari la zimamoto na uokoaji kwa Jiji la Dodoma.
Baada ya maelezo hayo Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma lilikubali kwa kauli moja kuanza hatua za awali za mazungumzo ya ushirikiano huo.
Jiji la Nagai lipo katika Jimbo la Yamagata likiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 214.67, shughuli kubwa za kiuchumi zikiwa ni kilimo na viwanda vyepesi vya vifaa vya umeme na viwanda vya madawa.
Baadhi ya waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wakiwa katika kikao cha kawaida cha Baraza hilo leo 29/04/2022.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.