Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassan amekabidhi pikipiki 14 kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Kata za Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino na kuielekeza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuendeleza utaratibu wa kuwapatia wataalam hao nyenzo ya usafiri ili kuwawezesha kuwafikia wanawake wengi kwa urahisi hasa wa vijijini ili wanufaike na fursa za kukua kiuchumi.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan alikabidhi na kutoa agizo kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto alipokuwa akizindua Mradi wa Kutokomeza Vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji dhidi ya Wanawake na Watoto kwenye Masoko nchini, tukio lililofanyika jijini hapa leo.
Mradi wa kutokomeza vitendo vya unyanyasaji na udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto kwenye masoko unaratibiwa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.