MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango ametoa maelekezo kumi yatasaidia kuimarisha sekta ya nyuki ili iweze kuchangia mapato ya Serikali na kwenye uchumi wa taifa kwa ujumla
Mpango ametoa maelekezo hayo kwa wadau mbalimbali wa sekta hiyo kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya nyuki duniani iliyofanyika jijini Dodoma ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, yeye mwenyewe na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda wamepewa tuzo maalum na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuthamini na kutambua mchango wao kwenye sekta.
Katika maelekezo yake ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana Wizara ya TAMISEMI kuyatambua maeneo maalum yenye fursa za kipekee katika eneo la mkoa wa Dodoma na Singida ili kuyahifadhi kisheria na kuwaelimisha wananchi wanaoishi katika maeneo hayo ambayo yana sifa ya uoto wa vichaka vya Itigi ambavyo duniani vinapatikana Tanzania na Zambia pekee.
Dkt. Mpango ameitaka Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) na Mfuko wa Misitu nchini(TAFF) kuwawezesha wananchi kwa kuwapatia mafunzo ya ufugaji nyuki na kuwapatia mizinga ya kisasa ili waweze kufuga kisasa.Pia ameelekeza Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania(TAFORI) kufanya tathinini mpya ya sekta ya Misitu na Nyuki ili kujana mipango ya kuendeleza sekta hizo.
Aidha, ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na wadau wa sekta hiyo kuja na mpango maalum wa ufugaji wa nyuki,kuendeleza program ya upandaji wa miti ambapo pia ameelekeza TAMISEMI kupitia Halmashauri zake zenye fursa ya ufugaji nyuki kote nchini kuajili wataalam watakao toa huduma ya ugani kwa wananchi na Wizara inayohusika na Kilimo kuandaa mkakati wa uchavushaji katika mazao.
Kuhusu Wizara ya Fedha , Dkt. Mpango ameitaka kuandalina namna ya kupunguza kodi kwenye vifaa katika mnyororo wa uchakataji wa asali, huku pia akiielekeza Wizara inayohusika na Mambo ya Nje kuzielekeza Balozi za Tanzania katika nchi mbalimbali duniani kutafuta masoko ili kupata fedha za kigeni.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.