Na Getruda Shomi, DODOMA
OFISI ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameshiriki katika kampeni ya kuhamasisha udhibiti wa taka ngumu kwa kuonesha utenganishaji wa taka ili kupunguza uchafuzi wa mazingira utokanao na kemikali za sumu katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma.
Akiongelea kampeni hiyo Afisa Mazingira katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Ally Mfinanga alisema kuwa ni muhimu kutunza taka kwa kuzitenganisha taka zinazooza, taka hatarishi na taka zinazoweza kurejerezwa hivyo itasaidia Halmashauri kuweza kuchakata taka zinazooza ili kutengeneza gesi kwaajili ya nishati lakini pia kwa taka zinazooza kutengenezea mbolea.
Akijibu swali la Mfanyabiashara wa Soko Kuu la Majengo, aliejitambulisha kwa majina Issa Ramadhani lililouliza ni wapi wanaweza kuuza taka ngumu kama chupa za maji safi baada ya kuzitumia, Mfinanga alijibu kuwa Jiji la Dodoma linawafanyabiashara wengi wanaonunua chupa hizo kwaajili ya kuzirejereza viwandani, hivyo alliwashauri wafanyabiashara wazipeleke huko kwani hununuliwa hivyo kujipatia kipato “Tunawafanyabiashara wengi ambao wananununa chupa za plastiki hivyo pelekeni huko na wanazinunua kwa shilingi mia na hamsini kwa kilo” alisema Mfinanga.
Akiongelea suala la udhibiti wa taka za kielektroniki, Afisa mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Agnes Mabina alisema taka hizo zitengwe na yapo makampuni yaliyosajiliwa na serikali kwaajili ya kukusanya taka hizo na kuzisafirisha nje ya nchi kwaajili ya kuziteketeza na zingine kurejerezwa. “Kuna viwanda maalum ambavyo vinarejereza taka hatarishi za kielektroniki ambapo zipo nje za nchi, hivyo yapo makampuni yameomba kibali kwaajili ya kuzikusanya na kuzipeleka nje ya nchi ambapo kuna viwanda vya kuzirejereza” alisema Mabina.
Naye mwalimu wa shule ya sekondari ya Makutupora, mwalimu Mohamed Mbwana baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo vya kutunzia taka kwa kuzitenga aliwahakikishia Maafisa mazingira hao kuwa watazitumia kwa uzuri kabisa wakifuata elimu ya namna ya kuzitenga taka hizo.
Kampeni hiyo inayooanza kufanyika Jiji la Dodoma inategemeway kufanyika pia katika mikoa mingine nchini Tanzania.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.