Na. Dennis Gondwe, DODOMA
KAMATI ya Siasa ya Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Dodoma imeridhika na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa maabara katika Shule ya Sekondari Makutopora na kuagiza ujenzi huo kukamilika ifikapo tarehe 28 Februari, 2023.
Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma, Charles Mamba alipoongoza Kamati ya Siasa ya Halmashauri kuu ya CCM kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa maabara moja katika Shule ya Sekondari Makutopora iliyopo jijini Dodoma.
Mamba alisema “nimeridhika na mradi huu wa ujenzi wa maabara unaendelea vizuri. Mjitahidi ikifika tarehe 28 Februari, 2023 mradi uwe umekamilika”.
Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa maabara katika Shule ya Sekondari Makutopora kwa Kamati ya Siasa ya Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Dodoma, mwakilishi wa Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mwalimu Fredrick Mwakisambwe alisema kuwa tarehe 28 Desemba, 2022 shule ilipokea shilingi 60,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa maabara moja, ujenzi ulianza tarehe 12 Januari, 2023. “Kiasi cha fedha kilichotumika hadi sasa ni shilingi 34,328,500 na kiasi ambacho hakijatumika ni shilingi 25,671,500. Hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 80. Matarajio ya kukamilisha kazi ni tarehe 15 Februari, 2023. Hadi sasa hatujapata changamoto yoyote katika utekelezaji wa mradi” alisema Mwalimu Mwakisambwe.
Shule ya Sekondari Makutopora ilianzishwa mwaka 2000 ikiwa na walimu 6 na wanafunzi 67, kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 772 kati yao wavulana 356 na wasichana 416. Shule inajumla ya walimu 44 kati yao wakiume 24 na wakike 20.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.