RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 01 Julai, 2021 amekabidhiwa taarifa ya maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti, 2022 kutoka kwa Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa.
Dkt. Chuwa amesema Sensa ya mwaka 2022 itatumia teknolojia ya kisasa ya kidijitali chini ya mfumo uliopo wa Serikali katika ngazi zote za Utawala kwa pande zote za Muungano na Sensa ya majaribio itafanyika mwezi Agosti mwaka huu (2021) katika mikoa saba kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.